WIZARA ya Afya nchini Hispania imetangaza kuwa viwanja vya soka vitaanza kujaa kama ilivyokuwa kabla ya janga la Corona na hiyo ni habari njema wa mashabiki wa La Liga.
Ni kwa maana hiyo, Wizara itaondoa utaratibu uliopo, ambapo kila kiwanja kinapaswa kuingiza asilimia 40 tu ya uwezo wake.
Kwa mujibu wa Wizara, kuanzia Oktoba mosi, mwaka huu, viwanja vyote vitakuwa huru kuingiza mashabiki kulingana na uwezo wake.
Hata hivyo, kila eneo halitazuiwa kuwa na utaratibu wake endapo litaaamua kuendelea na utaratibu wa kudhibiti idadi ya mashabiki viwanjani.