25.6 C
Dar es Salaam
Thursday, October 28, 2021

Benzema aikisha mabao 72

KARIM Benzema alifunga bao pekee la Real Madrid jana, ingawa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ulimalizika kwa vigogo hao wa La Liga kutandikwa mabao 2-1 na Sheriff Tiraspol.

 Sasa, Benzema amefikisha mabao 72, hivyo kukaa nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote Ligi ya Mabingwa, akizidiwa na Cristiano Ronaldo (135), Lionel Messi (121), na Robert Lewandowski (75).

Msimu huu umekuwa mzuri kwa Mfaransa huyo kwani ameshazipasia nyavu mara nane na kutoa ‘asisti’ saba katika mechi saba tu za La Liga.

Rekodi zinazonesha kuwa hakuna mchezaji raia wa Ufaransa aliyewahi kufunga mabao mengi kuliko Benzema kwani hata Thierry Henry aliishia 50.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,502FollowersFollow
523,000SubscribersSubscribe

Latest Articles