29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Makamu wa Rais afanya harambee, Milioni 138 zapatikana

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, ameendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la Parokia ya Mwili na Damu ya Bwana Yesu Kristu katika taarafa ya Mwamashimba Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza litakalokuwa na uwezo wa kubeba waumini zaidi ya 1,000.

Katika harambee hiyo, jumla ya Sh milioni 138 zimekusanywa ambapo fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 116 zikitolewa huku ahadi ikiwa ni Sh milioni 22.

Lengo la harambee hiyo ilikuwa ni kukusanya kiasi cha Sh milioni 430 ambazo zinalenga kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Mungu Mwamashimba.

Akizungumza katika harambee hiyo kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdor Mpango, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Mizengo Pinda akatumia fursa hiyo kuzishauri taasisi za dini kuepuka migogoro kwa kukatia hatimiliki za maeneo yao.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu Jimbo kuu la Mwanza, askofu Renatus Leonard Nkwande ameipongeza Serikali kwa kuendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kujenga Umoja na mshikamano wa nchi bila kubagua dini wala kabila la mtu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles