28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

IWPG: Jamii ipewe elimu kuhusu amani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Ukosefu wa elimu kuhusu Amani imetajwa kama moja ya sababua inayochochea maeneo mengi duniani kuwa na machafuko jambo ambalo linatakiwa kupigwa vita na kila mtu.

Hayo yamebainishwa Jumamosi Agosti 26, 2023 na wadau wa Amani katika Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Amani wa Viongozi Wanawake duniani ulioandaliwa na Taasisi ya International Women’s Peace Group (IWPG) ambao umefanyika kwa njia ya mtandao ukihusisha washiriki zaidi ya 450 kote duniani.

Mkutano huo ulikuwa na kaulimbiu ya: Mabadiliko na uvumbuzi kwa nafasi ya wanawake wa Kizazi Kipya na siku zijazo.

Mmoja wa washiriki hao, Stella Palare amesema kuwa ni bayana wanawake duniani wanapaswa kupewa elimu juu ya Amani hatua ambayo amesemsa kuwa itasadia kutatua migogoro mbalimbali.

“Ni wazi kuwa elimu kuhusu Amani inahitajika sana hususana kwa wanawake ili kuhakikisha kwamba jamii yetu na dunia kwa ujumla inakuwa mahala salama pa kuishi kwani tunaamini kwamba iwapo mwanamke atapata elimu kuhusu Amani basi ni bayana kuwa kutakuwa na Amani duniani kote.

“Elimu kuhusu Amani inapswa kuanzia nyumbani kwa kuwafundisha watoto wetu, shuleni na jamii kwa ujumla hivyo hili ni jukumu la kila mmoja wetu kujenga jamii yenye Amani,” amesema Stella.

Akichangia katika mjadala huo, Mkanibwa Magoti Ngoboka ambaye ni Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha na Mkurugenzi Mendaji, Community Actions and Empowerment Tanzania, na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya IWPG Iringa Tanzania, amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinaendelea kueneza elimu kuhusu Amani.

“Kama tunavyofahamu kwamba Tanzania ni moja ya nchi ambazo IWPG inatawi katika kuhakikisha kuwa mani inapatikana, katika hili niseme kwamba tunajipongeza kwa hatua ambazo tumeendelea kuzichukua, jambo la kufurahisha zaidi ni mashindano ya amani ambayo yamekuwa yakifanyika nchini ambapo mmoja ya washindi wa mashindano haya ya Amani ni shule ambayo inatoka mkoani Iringa.

“Hivyo, juhudi zinaendelea kuhakikisha kuwa tunakuwa na jamii yenye Amani kwani kwa kufanya hivyo ndipo kutakuwa ni chachu ya dunia nzima kuwa na Amani, hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anashiriki kikamilifu kuleta Amani popote pale alipo,” amesema Mkanibwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa IWPG, Hyun Sook Yoon amesema Amani haipaswi kuwa jambo la mtu mmoja tu badala yake inapaswa kuwa jukumu nla kila mmoja wetu katikia kufakikisha kuwa dunia inakuwa mahala salama pa kuishi.

“Jambo la Amani siyo la mtu mmoja badala yake tunapaswa kushikamana sote katika kuhakikisha kuwa tunahimiza Amani kote duniani. Hivyo wanakwake kama nguzo muhimu katikia familia wanao wajibu wa kuanza kuijenga Amani katika ngazi ya famia hatua ambayo itachochea na jamii kuwa na Amani hatimaye taifa na dunia kwa ujumla,” amesema Hyun.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles