29.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaanza kukabiliana na uhaba wa dola nchini

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Serikali imeanza kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa dola ambayo imekuwa ikisababisha kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali nchini ikiwamo mafuta ya petroli.

Hayo yabainishwa Dar es Salaam Agosti 26, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ambapo amesema kuwa Serikali imeanza kukabiliana na changamoto hiyo kwa kununua dhahabu ambapo mpaka sasa imenunua kilo 400.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Amesema pamoja na hayo Serikali pia imeanza kutafuta mikopo itakayoongeza dola pamoja na kuwapatia wafanyabiashara Shilingi na wao kutoa Dola.

“Tunatoa dhamana kwa biashara zinazouzwa nje ili tuweze kupata dola yaana mabenki yanawapa wafanyabiashara kwa kuchangia asilimia 50,” amesema Msigwa.

Aidha, Msigwa ameongeza kuwa bado wanaendelea na utaratibu wa Benki kuu (BOT) kuuza dola kwa jumla kwenye mabenki ambayo inakuwa imeshuka bei ili mabenki yote yawe na dola na yapunguze viwango vya kubadishia dola kwa wananchi.

“Tunaendele kutoa leseni kwa wanaotaka kufungua maduku ya kubadilisha fedha,” amesema Msigwa.

Msigwa amesema zaidi ya leseni 80 zimetolewa kwa wafanyabiashara hivyo ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kuomba leseni hiyo kwa kuzingatia masharti mapya ya leseni.

Amewataka wananchi kuongeza juhudi katika uzalishaji wa bidhaa ili kuongeza mauzo nje ya nchi hali itakayosaidia upatikanaji wa Dola.

Akizungumzia kuhusu miradi na kimkakati mbalimbali Msigwa amesema Serikali kwa kushirikiana na Shirikaa Reli Tanzania (TRC) wanaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa awamu ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi mwanza km 1,219 na awamu ya pili kutoka Tabora hadi Kigoma km 506.

Amesema thamani ya mradi huo mpaka sasa ni Sh Trilioni 23.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles