25.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 6, 2024

Contact us: [email protected]

Majaribio ya miundombinu ya mradi wa maji Butimba yaendelea

*Utekelezaji wake uanenda kwa kasi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Neli Msuya pamoja na timu ya Wataalamu wa Sekta ya Maji iliyoundwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Agosti 21, 2023 imefanya ziara ya kukagua mradi wa maji Butimba.

Ziara hiyo imetokana na kikao kazi baina ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na timu ya Wataalamu wa Sekta ya Maji kilichofanyika Agosti 24, 2023.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Msuya amesema muitikio wa mkandarasi ni mzuri na kwamba baadhi ya miundombinu ndani ya mradi imeanza kufanyiwa majaribio lengo ikiwa kuhakikisha ifikapo Septemba 15, mwaka huu majaribio ya mradi mzima yanafanyika.

“Tumetembelea kuangalia mradi wa maji wa Butimba na tunafurahi kwamba utekelezaji wake unakwenda vizuri, Mkandarasi anajitahidi sana na nimatumaini yetu kwamba mradi huu utakamilika ndani ya muda uliopangwa,” amesema Msuya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles