23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Makala: Marlaw afunguka kuhusu Muziki, maisha yake

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Unamkumbuka Marlaw? kama haumkumbuki nitakukumbusha kwa uchache. Huyu ni Msanii aliyewahi kutamba na ngoma kali kama Bembeleza, Bado umenuna, Daima na Milele na nyingine nyingi.

Marlaw ambaye jina lake halisi ni Lawrence Malima, pia anafahamika kama mume halali wa Staa wa Zamani wa Bongo Fleva, Besta Malila, ambaye amejaaliwa kupata naye watoto watano wakiume watatu na wa kike wawili.

Mtanzania Digital imepata wasaa wa kuzungumza na Marlaw ambaye ni mtoto wa tano katia ya watoto sita wa Mzee Malima, kuhusu mambo mbalimba,i ikiwamo muziki wake na maisha kwa ujumla.

Mtanzania Digital; Mambo vipi Marlaw

Marlaw; Poa

Mtanzania Digital; Kitambo tangu Bembeleza hadi leo unawatoto wangapi?

Marlaw; Familia kubwa sasa hivi nina watoto watano, wakike wawili na wakiume watatu wakwanza ana miaka 11 na wa mwisho anamika miwili.

Mtanzania Digital; Ndoa yenu ina muda gani hadi sasa?

Marlaw; Ndoa yetu hadi sasa itakuwa inamiaka 10 na tunatarajia kufanya sherehe ya kutimiza miaka kumi ya ndoa yetu.

Mtanzania Digital; Maisha ya Marlaw yapoje kwa sasa?

Marlaw; Maisha yako poa na yanaendelea vizuri, Baba wa familia na si baba tu ni zaidi ya mzazi ambaye nikiwa sipo watoto wananitafuta na kunitaka nirudi haraka.

Mtanzania Digital; Unafanya kazi za nyumbani?

Marlaw; Ndio kwa nini nisifanye kazi nafanya cha kwanza mimi ni baba kitendo cha kuwa baba tayari ni kazi tosha kwa kuwa ndio mwangalizi wa kwanza wa familia, lakini nafanya shughuli zingine kama kufua kuosha vyombo, kufanya usafi na kukata majani nje ya nyumba sio kila siku anafanya mama peke yake tunasaidiana.

Mtanzania Digital; Unajua kupika?

Marlaw; Ndio najua kupika na napikaga vyakula tofauti tofauti kama wali na ugali na kuandaa chakula wakati mwingine mke wangu anapumzika.

Mtanzania Digital; Unapenda chakula gani?

Marlaw; Nilikuwa napenda kula chipsi, nyama na vinyaji lakini kwa sasa nimepata elimu ya afya kuhusiana na magomjwa hivyo sili vyakula ninavyotaka mimi nakula vyakula vinavyohitajika kula.

Mtanzania Digital; Muda wako unapokuwa una kazi unautumia kufanya nini?

Marlaw; Ninapokuwa sina kazi nautumia kufanya mazoezi, ili kuimarisha mwili na wakati mwingine kucheza na watoto au kuperuzi mitandaoni nijue ni kitungani kinaendelea duniani.

Mtanzania Digital; Unafanyanga Shoping ya nguo na mahitaji kwa muda gani?

Marlaw; Kwa sasa nipo na familia nafanya shoping karibia kila siku kwa kuwa nina watoto unakuwa unanunua vitu mara kwa mara mahitaji yanaongezeka, tofauti nilivyokuwa nakaa mwenyewe, mara nyingi nilikuwa nafanya shopingi kwa ajili ya kupata nguo za shoo.

Mtanzania Digital; Mavazi gani unapendelea kuvaa?

Marlaw; Sina mavazi maalumu huwa navaa kutokana na tukio lilivyo na ninapokwenda naweza kuvaa tisheti na jinsi au hata suruali ya kitambaa na kama ni kutembelea sehemu maalumu naweza kuvaa suti kabisa, kwa kifupi napenda kuvaa nguo nzuri itakayonipendeza.

Mtanzania Digital; Unapendelea kwenda maeneo gani kupunguza mawazo na marafiki au wife?

Marlaw; Napenda kwenda sehemu yoyote inategemea na siku ilivyo tunaweza kwenda Beach kupunga upepo au kufanya shoping na wakati mwingine tunatembelea hata mbuga za wanyama ili kufurahi na family na kupumzisha akili.

Mtanzania Digital; Unafanya kazi gani tofauti na mziki?

Marlaw; Kazi zangu zote ninazozifanya zinahusiana na muziki bila muziki hakuna kazi nafanya zote ninazofanya zilisababishwa na Sanaa yangu.

Mtz Digital; Una mpango wa kuja kuwa mwanasiasa?

Marlaw; Hapana sina mpango wala sijawai kuwa mwanasiasa nitawapa ushirikiano kwenye kuwaimbia lakini sio mimi kuwa mwanasiasa kwa kuwa kuwa mwanasiasa ni kazi kubwa inayoitaji muda na uwanja wangu sio mkubwa kwenye siasa.

Mtz Digital Tofauti na Sanaa urafiki wako upojea?

Marlaw; Naongea na kila mtu na mi rafiki wa kila mtu uwa sichagui rafiki hata kwa wasanii kwangu wote ni sawa hakuna alie mzidi mwenzake kwangu zaidi, rafiki yangu kipenzi ni mkewangu Besta.

Mtanzania Digital; Unajivunia kitu gani kupitia kazi zako?

Marlaw; Hadi sasa natimiza miaka 13 tangu niingie katika tasnia ya Bongo Fleva japo kuwa nimetoka kwenye familia ya waimbaji wa nyimbo za Injili peke yangu nikatoka kwenye nyimbo hizi lakini ndugu zangu wote ni waimbaji wa injili.

Mtanzania Digital; Maroo asanye sana kwa muda wako.

Marlaw; Asante na wewe kwa kutimiza majukumu yako ya kazi hisiwe mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles