22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Washiriki 18 wa shindano la Bingwa kuingia kambini

Na Brighiter Masaki, Mtanznaia Digital

Washiriki 18 wametinga katika Msimu wa Kwanza wa Shindano la Bingwa litakalorushwa kupitia TV3 katika King’amuzi cha Startimes.

Shindano hilo la Bingwa lilifunguliwa hivi karibuni na kukutanisha watu mbalimbali maarufu wenye ushawishi katika jamii.

Ambao walipendekezwa katika ukurasa wa Mtandao wa kijamii wa Instagram wa StarTimes nakutakiwa mashabiki wao kuwapigia kura za kutosha ili kuwawezesha washiriki 16 kuingia katika jumba la bingwa rasmi.

Akizungumza na Waandishi Wahabari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Julai 13, 2021 Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa, amesema awali walikua washiriki 23 ambao waliweza kupendekezwa na hatimae kuingia kwenye mchakato wa kupigiwa kura za kutosha ili waweze kuingia kambini rasmi.

“Kupitia chaneli ya Tv3 kwenye kng’amuzi cha Startimes tumeweza kushirikiana kwa pamoja na kuona kwa jinsi gani washiriki 18 walipigiwa kura kwa haki na ndio hatimae tumewapata na wataingia kambini kwa ajili ya kuwania fedha tasrimu Sh milioni 10 pamoja na gari ambalo kwa sasa hatuliweki bayana,” amesema Malisa.

Aidha, Malisa ameongeza kuwa Reality Shoo hiyo itatazamwa na watu kuanzia umri wa miaka 15 kutokana na kuwepo vitu vingi kuanzia Burudani na Elimu.

“Zawadi kwa mshindi atakaepatikana kwenye Shindano la Bingwa atajishindia kitita cha Sh milioni 10 pamoja na gari huku washiriki wengine wakipewa kifuta jasho,” amesema Malisa.

Kwa mujibu wa Malisa, washiriki hao walioingia kambini watalala kwa muda wa siku 60 bila simu za mkononi na watajifunza vingi wawapo kambini hapo.

Kwa upande wake Msanii wa vichekesho, Idris Sultan, amesema yeye kama mwongozaji wa shindano hilo anaamini watampata bingwa bora kwa sababu ni washiriki hao ni miongoni mwa watu wenye ushawishi chini.

“Watakaa kwenye jumba la Bingwa kwa miezi miwili wakiwa hawana simu wala mawasiliano na watu wa nje na kila wiki watakuwa wakitoka washiriki watano hadi atakapopatikana mshindi,” amesema Su;tan.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki, msanii Harmorapa amesema amejipanga kuwa mshindi wa shindano hilo na anatarajia kushinda kwani hadi sasa hajaona mshindani wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,169FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles