27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Alikiba, Diamond Platnumz kuwania tuzo za BoomPlay

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Zaidi ya Wasanii tisa wa Muziki wa Bongo Fleva nchini watapokea tuzo wiki hii kwa kuvunja rekodi ya kuwa na wasikilizaji wengi kupitia Programu tumishi(APP) ya Boomplay.

Tuzo hizo maarufu kama ‘Boomplay Plaques’ hutolewa mara moja kila mwaka ili kutambua jitihada za wasanii wanaofanya vizuri kwenye App hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa tuzo hizo kutolewa ambazo ni mahsusi kwa wasanii ambao wameendelea kufanya vizuri kupitia kazi zao za muziki ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Akitoa taarifa ya tuzo hizo, Meneja Mkuu wa Boomplay nchini Tanzania, Natasha Stambuli amesema miongoni mwa wasanii watakaowania tuzo hizo ni pamoja na Diamond Platinumz, AliKiba na Harmonize.

“Wasanii kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Rayvanny, Nandy, Mbosso, Zuchu, Aslay na Darassa ni baadhi ya wale ambao wameendelea kuvunja rekodi kupitia App ya Boomplay na nifuraha yetu kuwatambua na kuwapa tuzo.

“Pamoja na mambo mengine ambayo tumeendelea kushirikiana na wasanii wetu, huu ni uthibitisho wa dhamira yetu endelevu ya kuhakikisha kuwa tasnia ya muziki inaendelea kukua na kusonga mbele,” amesema Natasha na kuongeza kuwa:

“Kama kampuni inayoongoza kwenye utoaji wa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki Afrika siku zote tumekuwa mstari wa mbele katika kutambua wasanii waonaendelea kufanya vizuri kwa kuvunja rekodi mbalimbali kupitia kazi zao za muziki. Matarajio ya Kampuni ni kuona wasanii wengi zaidi wanapata tuzo hizi kila mwaka,” Natasha.

Stambuli ameongeza kuwa vigezo vilivyotumika kuchagua wasanii ni pamoja na wingi wa usikilizwaji (Streams) wa wimbo wa msanii husika, albamu na usikilizwaji unaotokana na ujumla wa nyimbo za msanii. Takwimu za washindi zimechukuliwa kuanzia mwezi Novemba 2020 hadi Mei 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles