22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Simba kwenda Kigoma na kombe lao

Winfrida Mtoi

Bodi ya Ligi, imesema itaikabidhi timu ya Simba kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Jumapili, Julai 18,2021 itakapocheza na Namungo kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Wekundu wa Msimbazi hao walifanikiwa kutetea ubingwa huo kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuifunga Coastal Union mabao 2-0 na kufikisha pointi 79 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote.

Bodi ya Ligi imeipongeza Simba kwa kutwaa ubingwa huo, pia timu zote zilizoshiriki kwa kuendelea kuonesha ushindani ulisaidia kuongeza ubora wa michuano hiyo na kushika nafasi ya nane Afrika.

“Simba watakabidhiwa kombe hilo na medali baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa mwisho dhidi ya Namungo,” imesema bodi hiyo.

Baada ya kumaliza mechi ya mwisho ya ligi, Wanamsimbazi hao wanakabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga utakaopigwa Julai 25, 2021, mkoani Kigoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles