23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii nchini watakiwa kutumia fursa zinazotolewa na wadau

Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Wasanii watakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na wadau wa Sanaa ili kusaidia kukuza na kutangaza kazi zao kupitia mafunzo wanayoyapata.

Akizungumza na Mtanzania Digital mapema leo Julai 12, 2021 Dar es Salaam, viwanja vya Nafasi Art Space, Afisa Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Adelina Bumbaru, amesema kuwa amefurahishwa na mafunzo yanayotolewa na Ubalozi wa Swizland yanayowasaidia wanasanii.

“Kazi za sanaa zinahitaji kuwekeza tunapopata ushirikiano wa watu au makampuni mbalimbali, yanasaidia kwetu tunasikia furaha kwa kuwa inatoa fursa kwa wasanii wetu.

“Msanii anapopata sapoti tunafurahi kwakuwa msanii wa Tanzania akifanikiwa na baraza linafanikiwa pia kwa tunashukuru ubalozo wa Swizland kwa kutoa fursa kwa wasanii wetu,”amesema Adelina.

Kwa upande wake Balozi wa Swizland nchini, Deshar Sor amesema wanawasapoti wasanii wa Tanzania kwa takribani miaka mitano na sasa wanatoa nafasi kwa wasanii kuwa huru kujieleza kwenye maswala ya sanaa na kuweza kuwasaidia.

Naye Mratibu wa Sanaa za maonyesho, Kwame Mchaulu, kutokea Nafasi Art Space amesema kuwa nafasi ni sehemu ya jamii kujifunza kuhusu sanaa na kunamisaada tofauti kwa wasanii.

“Tulikuwa na mjadala wa kujieleza kwa kujuwa kuwasaidia na wasanii kwa ushirikiano wa Uswizz kusapoti wasanii kupitia Nafasi Art Space, kuomba kupata udhamini wa miradi yao inayohusu sanaaa mbalimbali,” anasema Chaulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles