23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AELEZA MKAKATI WA DAWA

Na Mwandishi Wetu-LINDI


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ununuzi wa dawa na vifaa tiba na kwamba hakuna mgonjwa atakayekwenda kutibiwa katika hospitali, vituo vya afya au zahanati  bila ya kupatiwa dawa.

Ameyasema hayo juzi alipokuwa akizungmza na wananchi wa Wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Wilaya.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe, Mary Majaliwa  katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Lindi, alisema Serikali haitaki kusikia wananchi wanakwenda hospitali, vituo vya afya au zahanati na kukosa dawa.

Alisema moja kati ya ajenda muhimu ya Serikali ya awamu ya tano ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake, ambapo kila mwezi halmashauri zote nchini zinapelekewa fedha za ununuzi wa dawa.

“Serikali hii ya Rais Dk. John Magufuli inatoa fedha za kununulia dawa kila mwezi katika halmashauri zote nchini. Sasa kama hapa Liwale kuna malalamiko ya wananchi kukosa dawa katika hospitali yetu, Mkuu wa Wilaya kafuatilie huko halmashauri ili kujua wanapeleka wapi fedha za dawa,” alisema.

Katika bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka wa fedha 2017/2018, jumla ya Sh bilioni 236 zimetengwa kwenye ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles