29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Maagizo ya Mavunde yakiukwa mgodi wa Ikinibushiu Bariadi, wachimbaji wadogo walalamika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Licha ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde kuagiza Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Mgodi wa Ikinibushiu, wilayani Bariadi mkoani Simiyu wapewe leseni na wasiondolewe wala kunyanyaswa ikiwemo kuhakikisha haki zao zinalindwa, wachimbaji hao wamelelamikia vitendo vinavyofanywa na watu waliyopatiwa leseni za kumiliki eneo hilo kwa kutaka kuchukua maduara yao na kuwaondoa.

Itakumbukwa kuwa Januari, mwaka huu, mgodi huo uliuwa watu 23, kwa kufukiwa na udogo wakati wakiwa ndani ya mashimo wakichimba dhahabu, hatua ambayo ilimfikisha Waziri wa Madini katika eneo hilo na kuzungumza na wachimbaji hao na kutoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha uchimbaji unaendelea kufanyika kwa kuzingatia usalama.

Aidha, Waziri Mavunde aliwahakikishi Wachimbaji hao kuwa haki zao za msingi zote zitalindwa ikiwemo kutoondolewa katika mgodi huo, ambao sasa wachimbaji hao wameeleza kushangazwa na vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa na Watu wanaodai kuwa ndio wamiliki wa eneo hilo.

Kwa mujibu Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu, Mayigi Makolobela akizungumza na Mtanzania Digital kwa simu, Afisa Madini alisema mgodi huo tayari Serikali imetoa leseni 2 kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kupewa kikundi cha Ikinabushu.

“Kama utakumbuka tarehe 12 mwezi uliyopita nilienda nikazuia shughuli za uchimbaji, lakini badae tukafunga mgodi lakini wakaendelea kuchimba na mnakumbuka tukapoteza watu 23. Niseme tu Serikali imetoa leseni 2 katika eneo hilo na tarehe moja mwezi huu Mkuu wa Mkoa aliikabidhi,” alisema Makolobela.

Hata hivyo, Wachimbaji wadogo wamekuwa wakilalamika kutozwa fedha kiasi cha Sh milioni 15 kila duara, kinyume na makubaliano ya Serikali na kwamba walivyohoji fedha hizo ni za kazi gani ndipo walipoitwa na kuojiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi.

Madai ya wachimbaji, hao ni baadhi ya viongozi wa Serikali wilayani humo, kushiriki kuwakandamiza, huku wakiwa wameruhusiwa na Waziri wa Madani kuendelea na uchimbaji katika eneo hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mmoja ya Wachimbaji hao, Yohana Makuru Sinta, alisema wamekuwa wakitishiwa mara kwa mara ikiwemo kukamatwa na kutishiwa kupewa kesi kutokana na wao kudai haki zao za kutaka waendelee kufanya shughuli zao za uchimbaji katika eneo hilo.

“Ndugu Waandishi wa habari sisi tuliamua kufuata utaratibu na kuamua kwenda kwa Mkuu wa Wilaya, tulifika na kufukuzwa, Lakini tulipofika tulipewa vitiso na kuzuiwa kuongeza na kila mtu aliandikisha na kuacha namba yake ya simu na kuambiwa uondokeni tutawafungulia kesi, Nilishanga Ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kutulikiza tuambiwa uwanja wa Halmashauri uko wapi, naulizwa mnada wangombe uko wapi kweli hii ni haki au unyanyasi na uongozi wa kutumia mabavu.”alisema Sitta.

Aidha, wachimbaji hao walimuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari Samia Suluhu Hassan kuutazama, mgodi huo, kwani katika mgodi huo wamepoteza ndugu zao sambamba na wakinamama waume zao na kutaka kuondolewa kwenye hayo maduara ili wamiliki wa leseni wayachukue kwa kutumia nguvu.

Elizaberth Samson ambye alipoteza ndugu katika mgodi huo akizungumza kwa uchuku huku akibubujikwa na machozi alisema, kimejitoikeza kikundi cha watu ambao wametumia njia za ujanja kupata leseni na kamba sasa wanataka kuwakandamiza kwa kuwaondoa.

“Hapa tuamenzisha mgodi sisi wananchi, tumehangaika hapa leo watu wanakuja na kutaka kutondoa tunaomba Mheshimiwa Rais atuone na atusaidie, mfano kuna mmoja ya Wakurugenzi anaejulikana kwa jina la Nhandi Nengero huyu anatuomba hisa kwa nguvu kwenye maduara yote kinyume na matakwa ya umiliki wa leseni,” alisema Samson.

Hata hivyo, baada ya waandishi wa habari kufika katika mgodi huo, Samuel Luhende ambaye ni Meneja aliwazuia kufanya kazi yao na kuhoji wamepata wapi kibali cha kufika hapo na kusababisha kuitwa na askari polisi waliyokuwa katika eneo hilo na kuwataka wasubiri utaratibu kutoka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bariadi na Mkuu wa Wilaya.

“Mmefika hapa kibali cha kuja hapa mmepata wapi, nani amewaruhusu, mlitakiwa kuniambia mimi ili nijue mmefuata nini hapa,”alihoji Luhende.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles