30.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Tin White, YJ wazichapa kavu kavu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

STAA wa vichekesho Bongo, Tin White, ameamua kuzichapa ngumi kavu kavu na msanii wa muziki wa Bongo Fleva anayefagamika kama YJ akidai malipo ya kazi yake ambayo mwimbaji huyo amekuwa akimzungusha.

Msanii YJ

Tin White, ameweka wazi kuwa YJ alimfanyisha kazi ya kuwa Video King lakini hakupewa malipo kama walivyokubaliana mpaka akaamua kufanya maamuzi hayo magumu ya kwenda nyumbani kwa YJ.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Msanii YJ amemshtumu Tin White kwa kusema kuwa alivamia nyumbani kwake na kufanya fujo ikiwa ni pamoja na kuvunja TV na simu jambo lililompa hasira.

“Kuna hela sikummalizia baada ya kufanya naye kazi lakini uamuzi aliofanya ni mkubwa sababu TV na simu yangu ni vitu vya gharama kubwa kuliko hata pesa anayodai ambayo kwangu mimi ni ya chai tu,” ametamba YJ anayetamba na wimbo Natamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles