26.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 26, 2022

LUPITA, RIHANNA KWENYE FILAMU MOJA

NEW YORK, MAREKANI


NYOTA ya msanii wa filamu nchini Marekani ambaye ni mzaliwa wa Kenya, Lupita Nyong’o, inazidi kung’ara baada ya kuweka wazi kwamba yupo kwenye maandalizi ya kufanya filamu ya pamoja na nyota wa muziki wa RnB, Robyn Rihanna.

Inasemekana kuwa, wawili hao walikutana mwaka 2014 kwenye mashindano ya urembo yajulikanayo kwa jina la Miu Miu, kisha walipiga picha ya pamoja na baada ya hapo mazungumzo yao yaligusia masuala ya filamu.

Licha ya muda mrefu kupita tangu walipokutana, lakini Lupita alijikuta akimkumbusha Rihanna mbali pale alipoweka picha waliyopiga pamoja na Rihanna walipokutana mwaka huo 2014, huku mashabiki wao wakiwapongeza kwa kupendeza.

Baada ya picha hiyo na kujali kwa mashabiki wao, Rihanna alimtaka Lupita wafanye kitu cha pekee kitakachowaongezea furaha mashabiki wao.

Ndipo wawili hao wakafikia makubaliano ya kufanya filamu ya pamoja inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni. “Picha ambayo niliiweka kwenye akaunti ya Twitter imetufanya mimi na Rihanna tufanye filamu, hivyo mashabiki wakae tayari kwa kazi yetu,” aliandika Lupita.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,803FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles