NE-YO AMPONGEZA DIAMOND

0
412

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Shaffer Smith (NE-YO) amempongeza staa wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul (Diamond) kwa kuzindua manukato yake yajulikanayo kama Chibu.

Ne-Yo, aliyeshirikishwa na Diamond kwenye wimbo wa ‘Marry You’, ameshindwa kuzuia hisia zake na kumpa pongezi msanii huyo kwa hatua aliyofikia ya kuwa na manukato yake, kama ilivyo kwa wasanii wakubwa nchini Marekani.

Ne-Yo amesema, hiyo ni hatua kubwa kwa msanii huyo katika biashara na amemtakia kila la heri katika biashara hiyo na mambo yake mengine.

Mbali na Ne-Yo, wasanii wengine waliomtumia pongezi Diamond kwa hatua aliyopiga ni pamoja na Kingsley Okonkwo (Kcee) kutoka nchini Nigeria na Jah Prayzah wa Zimbabwe.

Baadhi ya wasanii wakubwa duniani wenye manukato yao ni pamoja na Robyn Rihanna, Kelly Rowland, Sean Combs ‘Diddy’ Beyonce, 50 Cent na wengine wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here