25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 6, 2022

Contact us: [email protected]

LEICESTER CITY WAJA KIVINGINE

leicester-cityNa SAMUEL SAMUEL­-ARUSHA

WASWAHILI wanasema kupanga ni kuchagua. Hii ina maana kila mmoja ana malengo yake katika mustakabali wa maisha.

Msimu uliopita wa 2015-16 ndani ya Ligi Kuu England, Leicester City waliibuka mabingwa wa ligi hiyo, ikiwa ni mara yao ya kwanza na kuwashangaza wengi, baada ya kuwaangusha vigogo  kama Manchester United, Arsenal, Liverpool na Chelsea.

Harakati za kutwaa ubingwa huo ilikuwa ni mipango yao thabiti ndani ya ngome yao ya King Power Stadium. Tunathubutu kusema ilikuwa ni mipango yao kutokana na jitihada walizoziweka toka mwanzo wa ligi.

Msimu huu wakiwa ni mabingwa watetezi, lakini inaonesha malengo yao si kutetea ubingwa huo, baada ya kucheza mechi nane kabla ya ule wa mwishoni mwa wiki, huku wakiwa na alama 13 na pointi 8 katika msimamo wa ligi, wakishinda michezo 2 , sare 2 na kufungwa michezo 4.

Licha ya kutoonesha matumaini ya kutetea ubingwa wao ndani ya EPL, Leicester City inaonesha mpango wao msimu huu ni kufika mbali klabu bingwa Ulaya.

Tayari Leicester City wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka England kushinda mechi tatu mfululizo Klabu Bingwa Ulaya, lakini pia ikiwa timu ya tano Ulaya kushinda mechi zake tatu za mwanzo ligi ya mabingwa, wakitanguliwa na AC Milani, Paris St- German, Juventus na Malaga.

Kocha Mkuu wa Leicester City, Claudio Ranieri, anajinadi kuifikisha mbali klabu hiyo katika michuano ya klabu bingwa Ulaya, lakini pia hajakata tamaa kuingia nafasi nne za juu kwenye ligi kuu.

Ranieri anakwenda mbali zaidi kwa kusema wachezaji wake ni bora kwenye safu ya ushambuliaji, wakiongozwa na Vardy, ambaye msimu uliopita aliibuka kinara wa ligi kwa mabao 24, hivyo anaamini  hawatamuangusha kuendelea kutikisha nyavu za wapinzani Klabu Bingwa Ulaya.

Vardy mpaka sasa amecheza mechi 8 kabla ya mwishoni mwa wiki bila kutikisa nyavu. Leicester City wanaongoza kundi G baada ya kushinda mechi 3 na kufikisha pointi 9, wakifuatiwa kwa mbali na Copenhagen kutoka Denmark wenye pointi 4.

FC Porto wana pointi 4 pia na Club Brugge wanaburuza mkia baada ya kufungwa mechi zao zote 3.

Kasi hii ndani ya klabu bingwa Ulaya ndiyo inawafanya wachambuzi wa soka duniani, hususan nchini England, kuona mbwa mwitu hao wamepanga nguvu zao klabu bingwa kuliko ligi kuu kama mabingwa watetezi.

Kimbinu na kiufundi licha ya ubora wao, nguvu zao zinaonekana wazi kuwa wanazielekezea klabu bingwa, lakini msimu huu beki yao imeonesha kutokuwa imara kama msimu uliopita.

Kitendo cha kuruhusu kufungwa mechi nne kati ya 8 walizocheza inaonesha ni dhahiri wana beki dhaifu.

Claudio Ranieri amekaririwa hivi karibuni akisema wachezaji wake wanateswa na msongo wa mawazo ndani ya ligi kuu, kuliko utayari walionao wanapocheza klabu bingwa.

Saikolojia yao inashindwa kuhimili hali ya kukamiwa na wapinzani wao kama bingwa mtetezi.

Claudio Ranieri anakwenda mbali kwa kusema anajisikia vibaya kila anapofikiria matokeo ya timu yake ndani ya ligi kuu.

“Si vyema kwa bingwa mtetezi baada ya mechi 8 kuwa nafasi ya 13. Tunahitaji kuwa bora katika kila michuano ili kudhihirisha ubora wetu na kutimiza malengo yetu.”

Mechi ijayo Leicester City wanakutana na Tottenham katika michuano ya ligi kuu mwishoni mwa wiki hii,  ni mchezo ambao unaonekana kuwa mgumu kwao kwa kuwa watakuwa ugenini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,606FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles