30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hasheem Thabeet kurudi NBA Septemba

hasheem-thabeetBADI MCHOMOLO NA MITANDAO

NI ndoto za kila siku na kiu ya Watanzania kuona wanamichezo wao wakifanya vizuri na kulitangaza taifa katika mataifa mbalimbali.

Bado tuko nyuma sana katika michezo, lakini kizazi cha sasa kinaonesha dalili ya baadhi ya wanamichezo wakilitangaza taifa katika michuano mikubwa ya kimataifa.

Katika soka tunaona jinsi Mbwana Samatta anavyoonesha jitihada za kutaka kufika mbali ambapo kwa sasa anacheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika klabu ya Genk.

Jitihada zake ni wazi zinaonesha kwamba anaweza kufika mbali kwa kuwa ana tamaa hiyo. Hali hiyo inawafanya wanamichezo wengine kupambana.

Katika riadha tumeona Mtanzania Alphonce Simbu jinsi alivyofanya kwenye riadha katika michuano ya Olimpiki nchini Brazil.

Leo SPOTIKIKI inaangazia katika mchezo wa kikapu ambapo inamuangalia nyota wa nchini Tanzania ambaye anakipiga katika Ligi D ndani ya klabu ya Grand Rapids Drive ya nchini Marekani, Hasheem Thabeet.

Huyu ni nyota ambaye alitamba na kulitangaza taifa katika mchezo huo baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu ya NBA nchini Marekani katika msimu wa  2009 akiwa na timu ya Memphis Grizzlies.

Alifanya vizuri pia akiwa na timu ya Oklahoma City Thunder katika msimu wa 2012 hadi 2014, lakini baada ya hapo alionekana kushuka kiwango chake na kutupwa katika ligi ya kujiendeleza kwa ajili ya kupandisha kiwango ili aweze kurudi Ligi ya NBA.

Kwa nini alishuka kiwango?

Inasemekana asilimia kubwa ya wachezaji wa Kiafrika wakipata mafanikio makubwa wanakuwa wepesi kujisahau na kukumbuka kile ambacho wamekipata.

Hali hiyo inawafanya wachezaji kushindwa kudumu kwenye mchezo husika kwa kuwa wanaamini kuwa tayari wamefanikiwa.

Thabeet alikuwa miongoni mwa wachezaji wa aina hiyo ambao walipata mafanikio makubwa, lakini walilewa sifa na kuanza kufanya starehe, kitendo ambacho kilishusha kiwango chake.

Alipanga safari ambazo si za lazima kuja Tanzania wakati wenzake kipindi hicho walikuwa katika mazoezi makali ili waweze kurudi na kasi nyingine.

Kwa nini anarudi NBA?

Kushuka kwa kiwango kwa mchezaji huyo kuliwagusa Watanzania wengi, lakini wapo ambao walimshauri mema ili aweze kurudi katika ubora wake na kuonekana tena katika Ligi ya NBA.

Hicho ndicho ambacho kinaweza kutokea kwa sasa, mchezaji huyo amepambana vilivyo katika Ligi D na kuonekana kuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao wana kiwango cha hali ya juu kwa sasa katika Ligi hiyo.

Ligi D ni sehemu ya kwenda kupandisha kiwango, hivyo tayari mchezaji huyo amezigusa timu mbalimbali za Ligi ya NBA baada ya kuonesha uwezo wake katika baadhi ya misimu.

Kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kuonekana upya katika NBA, huku baadhi ya timu kama vile Los Angeles Lakers, The New York Knicks na Washington Wizards zimetajwa kuanza kumzungumzia mchezaji huyo.

“Nilikuwa najisikia vibaya kuona sina nafasi katika NBA na nakuwa shabiki pale timu kubwa zinapocheza, lakini hali hiyo imenifanya kupambana kwa nguvu kwa ajili ya kurudisha hali ya mwanzo na nashukuru kwa sasa nipo vizuri na chochote kinaweza kutokea,” alisema Thabeet.

Awali nyota huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa na majina makubwa kwa mwaka 2009, ambapo alishika nafasi ya pili nyuma ya wachezaji ambao wanafanya vizuri kwa sasa kama vile James Harden, Stephen Curry na DeMar DeRozan wakiwa Ligi D.

Kipindi hicho Thabeet aliweza kuwa na wastani wa pointi 8.6, huku rebounds akiwa na  6.2 na blocks 2.4 kwa dakika 22.2 na kuwa mchezaji wa Ligi D namba tatu ambaye aliweza kublock mara 117, akishika nafasi ya nne kwa kuzuia ambapo alizuia mara 101.3.

“Nipo tayari kuichezea timu yoyote ya NBA kwa kuwa lengo langu ni kuonesha uwezo, kwa sasa ninazidi kupambana ili niweze kupata timu na ninaamini muda mfupi ujao nitakuwa NBA, hasa katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Frank Matrisciano ni nani?

Huyu kwa sasa ndiye anayesimama katika mafanikio ya mchezaji huyo, hasa katika kuhakikisha anarudi katika Ligi Kuu ya NBA.

Matrisciano ni mwalimu wa kikapu wa kimataifa ambaye anadai kuwa ameamua kujitolea kwa ajili ya mchezaji huyo, hivyo atahakikisha anatimiza malengo yake.

“Sikuwa namjua Hasheem, lakini siku zote lengo langu ni kusaidia watu, hivyo ninawapa nafasi, nilikutana na mchezaji huyo wakati wa chakula cha mchana na nikamwambia kwamba nitakusaidia bila ya kujali chochote ambacho kinaongelewa.

“Nikamwambia kama ameamua kuja kwangu basi atakuwa na sababu, hivyo kuna uwezekana wa kuzifikia sababu hizo na muda mfupi utakwenda kubadilisha maisha yako, kikubwa ni kusubiri.

“Ninaamini alijua nini alikifanya na akaweka wazi kila kitu, hadi sasa mambo yanakwenda sawa na ndoto zake zitakamilika muda si mrefu,” alisema Matrisciano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles