24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bei ya korosho juu

koroshoNA Allly  Badi Kilwa

BEI ya  korosho kwenye  mnada katika   maghala ya  Chama Kikuu cha Mwambao Lindi,imepanda hadi Sh 3,810 kutoka  Sh 3,710 kwa kilo katika mnada wa kwanza.

Hayo  yamejitokeza  kwenye   mnada  wa  korosho  uliofanyika  katika  Chama  cha  Ushirika Tapwa  wilayani  kilwa  mkoani Lindi jana.

Akizungumzia hali hiyo,Meneja  wa  Chama Kikuu cha Kuuza na Kununua Mazao Mwambao, Hasan Vudu alisema tani  2,355 za korosho  zimeingizwa  kwenye  mnada  na  makampuni  zaidi ya  19  yalishiriki kwenye  zabuni

Vudu.

Alisema ushiriki  mzuri  wa  makapuni  kwenye  minada unachangia  kuwapo  bei  mzuri ya korosho  kwani unaleta  ushindani Kwenye  soko.

Kwa upande wake, mkulima Mohamedi Ismail mkulima  alisema  bei ya  korosho sasa  inatia  moyo  na  kurudisha  matumaini  kwa wakulima na  kuongeza  mori ya kufufua  mikorosho  iliyokufa kuhudumia na kupanda    mipya.

Alisema  ni  wajibu  wa  wadau  wa  korosho,wakiwamo  Bodi  ya Korosho  na  Mfuko  wa Kuendeleza  zao hilo (WFU), kusimama imara

Kwa  upande  wake, Sharifa Mokiwa  kutoka  Bodi  ya Korosho,aliwataka  wananchi  na wakulima wa  korosho  kukausha  korosho  zao  ili  kupunguza  unyevu ambao  unaweza  kusababisha zao kupunza  ubora  na  uzito  wa  korosho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles