24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

KUTANA NA MSICHANA MWENYE ‘UMRI UNAOYEYUKA’

UNAPOMTUPIA jicho la haraka unaweza kudhani ni mwanafunzi mdogo, lakini kiuhalisia Lure Hsu anakaribia siku yake ya 42 ya kuzaliwa.

Mbunifu huyu wa mavazi kutoka Taiwan, ameondokea kuwa nyota wa karibuni wa mitandaoni, ambaye amevuta maelfu ya watu kwa mwonekano wake wa ujana.

Anasema siri kuu ya mwonekano huo ulio tofauti na umri wake ni wingi wa maji anayokunywa kila siku pamoja na ulaji wa mboga za majani.

 

Lure kwa mara ya kwanza alianza kufahamika mitandaoni kupitia mdogo wake aliyemtangulia umaarufu Sharon Hsu.

Sharon (35) ambaye ni mcheza filamu, alimkaribisha Lure kuhudhuria onesho moja la burudani mwaka 2015.

Agosti ya mwaka huo, Sharon alitupia picha za dadake huyo katika ukurasa wake wa Facebook akimtakia mema kusherehekea miaka 40 ya kuzaliwa.

Hilo ndilo lililoleta mshtuko, pale mashabiki wa mwigizaji huyo  walipogundua umri halisi wa Lure, ambaye awali walidhani ni mdogo wa Sharon.

Walisema kwa sababu ya uso wake usio na mikunjo na mitindo yake alionekana msichana mdogo tineja, yaani wa umri wa miaka 13-19 hivi.

Lure haraka haraka akauvaa umarufu katika mitandao ya jamii kwa maelfu ya watu kuanza kufuatilia akaunti zake za mitandao ya jamii.

Akaunti yake ya Instagram ikajitwalia wafuasi wapya 230,000 ndani ya muda mfupi mno huku Facebook ikipokea ‘like’ kutoka watu zaidi ya 341,000 kwa kipindi kifupi.

Wiki hii picha za Lure zilitumiwa vyombo vingi vya habari nchini China na Taiwan vikiwamo Sohu na ET Today, ambavyo vilimuita kuwa ‘mungu wa kike mwenye umri unaoyeyuka’.

Wakati akihojiwa na jarida la Friday la Taiwan, Lure alifichua siri kuu ya mwonekano wake wa ujana kuwa ni kunywa maji kwa wingi pamoja na mboga za majani.

Lure anasema kuhakikisha mwili daima una maji ya kutosha ni kitu muhimu sana.

Lure anaeleza kwamba hunywa maji mengi kila siku na hujaribu kukaa mbali na vinywaji vyenye sukari kama Coke. Kinywaji pekee, mbali ya maji akipendacho ni kikombe cha kahawa nyeusi kila asubuhi.

Ni shabiki wa mlo wa mboga za majani na anasema hupendelea mlo wenye ladha nyepesi na huepuka baadhi ya michuzi mizito ya kuchovya ambayo husindikiza vyama au mikate kutokana na kiwango chao kikubwa cha nishati.”

Lure anawashauri wanawake kuhakikisha ngozi zao zinakuwa nyevu kila siku kwa sababu ngozi inapokuwa na maji ya kutosha, unakuwa huna haja ya kuogopa kuzeeka na kuwa na mikunyo.

Kivuli cha jua ni muhimu kwa Lure wakati wa kiangazi.

“Mara ngozi yako inapounguzwa na jua, inakuwa kavu. Mikunjo mikunjo midogo huweza kuonekana,” anabainisha.

Anaongeza kwamba hutumia virutubisho vya ziada kila siku ikiwamo vidonge ya Vitamin C na collagen vinavyomsaidia kuidumisha ngozi yake iendelee kuwa ya ujana.

Hata hivyo, licha ya kudai hujaribu kujiepusha na vinywaji au vyakula vyenye wingi wa sukari na kalori, inaonekana mara moja moja akifurahia chokoleta tamu tamu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles