24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kituo cha usambazaji teknologia Nyakabindi chaanza na viazi lishe, mkonge

Derick Milton, Simiyu

Taasisi ya utafiti wa kilimo nchini (TARI) kupitia kituo chake kipya cha usambazaji wa teknologia za kilimo kanda ya ziwa Mashariki kilichopo Nyakabindi Mkoani Simiyu imeanza kutoa mafunzo ya uzalishaji bora wa viazi lishe pamoja na zao la mkonge katika mkoa wa Simiyu.

Hatua ya taasisi hiyo imekuja kutokana na wakulima wa mkoa huo kutoyapata kipaumbele mazao hayo, licha ya kuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi ambapo sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kukosekana kwa elimu ya uzalishaji wa mazao hayo.

Taasisi hiyo imeanza kutoa mafunzo kwa maafisa ugani ngazi ya kijiji na kata wa mkoa huo pamoja na wakulima zaidi ya 50, ambapo Mratibu wa usambazaji wa teknolojia za kilimo kutoka TARI Mshagulei Ishika amesema kuwa wameanza na mazao hayo kutokana na kuwa kipaumbee cha mkoa huo.

Ishika amesema kuwa TARI inatoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa, ambapo maafisa ugani hao watakuwa na jukumu la kupeleka elimu hiyo kwa wakulima vijijini ili kuanza kuzalisha mazao hayo.

Amesema kuwa kituo hicho mbali na kutoa mafunzo yake ya kwanza tangu kianze kufanya kazi baada ya maonesho ya Nanenane mwaka huu, kinaendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji jinsi ya kuzalisha kisasa.

“Serikali iliagiza kituo hiki kiwe endeevu baada ya maonesho, leo haya ni mafunzo ya kwanza, tumeanza kufanya kazi, tunawaomba wakulima wa Simiyu, Mara na Shinyanga kuja kwa wingi kupata mbegu bora, pamoja na teknologia za kisasa,” amesema Ishika.

Ofisa Mfawidhi wa kituo hicho cha Nyakabindi Isabela Mrema amesema kuwa wakulima wengi wa Simiyu wamekuwa hawazalishi mazao hayo kutokana na kutokuwa na elimu ya jinsi gani ya kuvizalisha na kutokupata mbegu.

“Kwenye viazi lishe wakulima wa Simiyu wengi hawajui na hawana uwez wa kupata mbegu zao, ingawa wanalima viazi ila vile vitamu, kupitia kituo hiki mbegu zipo za kutosha na tumeanza kuwapa elimu, lakini hata mkonge bado hawajatambua fursa zake,” amesema Isabela.

Akifungua Mafunzo hayo Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mkwabi Mjungu amewataka washiriki kuzingatia mafunzo hayo ili kuweza kufikia lengo la mkoa katika mazao hayo ambayo ni mkakati wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles