23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu aliyejeruhiwa na mwanafunzi aruhusiwa kutoka hospitalini

Aveline Kitomary, Dar es Salaam

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kiagata iliyopo Butiama mkoani Mara, Majogolo Ngwalali (36) aliyejeruhiwa na mwanafunzi wa kidato cha tatu akiwa kazini ameishukuru Taasisi ya MOI kwa kumpatia matibabu mazuri kwa wakati.

Akizungumza baada ya kuruhusiwa kutoka MOI, Majogolo amewashukuru wahudumu wa Afya wote kwa kumpa huduma bora na sasa anaendelea vizuri.

“Kwanza ninawashukuru madaktari na wauguzi hapa MOI wamenuhudumia vizuri toka siku toka Septemba 24 nilipofika hapa saa sita usiku pili nawashukuru wahudumu wa kituo cha Afya Kiagata na Hospitali ya Mara ambako nilipata huduma za awali kabla ya kuja hapa”, amesema Majogolo.

Pia ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Butiama ambayo ilihakikisha anapata huduma kwa wakati ikiwa ni pamoja na kumtafutia usafiri wa ndege kufika jijini Dar s salaam.

Akisimulia namna alivyojeruhiwa Majogolo, amesema alijeruhiwa na panga na mwanafunzi wa kidato cha tatu akiwa katika ukaguzi wa kawaida wa watoro na watorokaji.

“Tulikuwa tunafuatilia watorokaji na watoro ndipo mwanafunzi wa kidato cha tatu aliponijeruhi kwa kunikata mkono kwa panga,” amesema Majogolo .

Akizungumzia afya yake baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali Majogolo amesema anaendelea vizuri tofauti na hapo awali ambapo alikuwa na maumivu makali.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha uhusiano MOI, Patrick Mvungi amesema Majogolo alipatiwa huduma  ya upasuaji wa dharura siku hiyo hiyo aliyowasili hospitalini hapo na kwamba hivi sasa ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya yake kuimarika.

“Tumemruhusu kwenda nyumbani kwani afya yake imeimarika na anaendelea vizuri atarudi baada ya wiki mbili jumanne kwenye kliniki zetu,” amesema Mvungi.

Majogolo alifanyiwa upasuaji mkubwa wa kurekebisha mishipa katika mkono wake wa kushoto ambao aliyojeruhiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles