26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Kimwanga aahidi kumaliza kero Makurumla

SARAPHINA SENARA (UoI) Na WARDA LUPENZA (TURDARCo)

DAR ES SALAAM

MGOMBEA wa udiwani Kata ya Makurumla kupitia CCM, Bakari Kimwanga, amewaomba wananchi kumchagua ili kuboresha miundombinu itakayosaidia kuepuka adha ya mafuriko kipindi cha mvua.

Kimwaga alisema hayo  wakati akizungumza na wananchi katika Mtaa wa Kagera ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake, akiomba ridhaa ya kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu kwa nafasi ya udiwani. 

Alisema malalamiko ya wananchi katika Mtaa wa Kagera yamekua ni maji na hii inatokana na kutokuwepo miundombinu inayopitisha maji kipindi cha mvua pamoja na maji taka katika mtaa huo wa Kagera.

“Sisi tuliopo Mtaa wa Kagera, mwananchi anayeishi nyumba zinazoitwa bondeni ingawa sipendi kutumia usemi huu analalamika kisa ni mfereji wa Mto China, lakini ndani ya kipindi kifupi tunakwenda kujenga kingo imara amabao imekua kero hasa kwa wakazi wa Kalifonia.

“Kila mfereji una changamoto zake lakini sisi kama  Chama Cha Mapinduzi tunawahidi ndani ya miaka mitano tutakwenda kutengeneza mchakato utakaosaidia kuimarisha na kujenga miundombinu pamoja na mifereji inayopitisha maji huku juu ili kuepuka adha ya mafuriko kwa watu hawa,” alisema Kimwanga. 

Alisema ujenzi wa kingo imara katika Mto China utasaidia kupunguza adha ya mafuriko jambo ambalo limekua adha kubwa kwa wakazi hasa wa Kalifonia.

Aidha, alizungumzia suala la huduma bora za afya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kupata madaktari bingwa na kusimamia upatikanaji wa dawa zote na kuimarisha miundombinu pamoja na gari ya uhakika ya kubebea wagonjwa.

“Chama Cha Mapinduzi kikishirikiana na mimi ndani ya miaka mitano tunakwenda kuhakikisha katika Hospitali ya Mianzini pamoja na Makurumla kunakuwa na madaktari bora na wa uhakikisha,  ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa katika hospitali hizi.

“Inasikitisha pale ndugu yetu anapoumwa unapokwenda Mianzini unaandikiwa rufaa unaambiwa mgojwa huyu hatakiwi kutibiwa hapa, anatakiwa kwenda kuonana na madaktari bingwa hivyo anatakiwa kwenda Mwananyamala na unapofika kule unatakiwa kwenda Muhimbili na jambo ambalo hatujaliomba siku mbili anapoteza maisha, maiti inazuiliwa kwa sababu anadaiwa. Niwaahidi hilo halitakuwepo,” aliongezea Kimwanga.

Alisema Chama Cha Mapinduzi kinakuja na bima bora ya afya kwa wananchi ili kuondoa adha kwa wauguzi na wagonjwa wanapokwenda kupatiwa matibabu na kusema hii itaanza mwakani kama watampatia ridhaa ya kuwa kiongozi.

Hata hivyo, alizungumzia suala la kujikimu kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuwa na utaratibu mzuri wa mkopo wa halmashauri utakaomsaidia kila mtu kukopa na kurejesha  bila fidia na  haiwezi kumuumiza mtu yeyote na kusaidia hasa wanawake kufanya biashara.

Alisema mikopo hiyo itasaidia wakina mama na watu wenye ulemavu kutokana na utaratibu ambao utawasaidia kupata kwa urahisi huku akidai vikundi hivyo vimeundwa kisiasa, atakwenda kusimamia utaratibu wa utoaji wa mkopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles