KINONDONI YAPATA RPC MPYA, KAGANDA AHAMISHIWA MAKAO MAKUU

0
545

JESHI la Polisi nchini, limefanya mabadiliko ya watendaji wake katika mikoa ya kipolisi Kinondoni na shinyanga.

Katika mabadiliko hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, amemteua Murilo Jumanne Murilo kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni akichukua nafasi ya Suzan Kaganda ambaye amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia  Makao Makuu ya Polisi.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabus Mwakalukwa, nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Simon Haule, ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu  wa Polisi wa Mkoa wa Mara.

“Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi,” ilisema taarifa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here