PROF. MBARAWA: WATAKAOTII SHERIA NDIYO WATAKAOLIPWA FIDIA

0
415

 

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imesema itawalipa fidia kwa mujibu wa sheria wananchi wote waliopisha ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Mwigumbi mkoani Shinyanga baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Mwigumbi – Maswa yenye urefu wa km 50.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Sh bilioni 61.

“Kila anayestahili kulipwa fidia atalipwa kama sheria inavyoelekeza na endapo kuna mwenye malalamiko juu ya hilo serikali ipo itamsikiliza,” amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi na Viongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wa mkoa ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na spidi inayotakiwa.

Naye, Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Shinyanga Injinia Batholomeo Ndirimbi, amesema tayari fedha zimetengwa kwa ajili ya ulipaji fidia na watahakikisha kuwa fedha hizo zinalipwa kwa watu sahihi wanaostahili fidia hizo.

“Tutasimamia zoezi hili kwa umakini na kutoa fidia kwa wale wote wanaostahili kisheria,” alisema Injinia Ndirimbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here