23.9 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaainisha mpango wa kusaidia wachimbaji wadogo nchini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameainisha mpango wa Serikali wa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Mei 9, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Dk. Christine Ishengoma Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga.

Ameongeza kwamba, mpango wa Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo wachimbaji wa madini wa Wilaya ya Ulanga unahusisha masuala mbalimbali ikiwemo kuwekeza zaidi katika utafiti wa kina kugundua uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo.

“Mhe. Spika maeneo mengine ni utoaji wa leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo; kutoa elimu ya matumzi ya teknolojia sahihi ya uchimbaji ili kuongeza tija; huduma ya uchorongaji kwa gharama nafuu kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),” amesema Waziri Mavunde.

Vilevile, amesema kuwa, mpango mwingine ni kuwezesha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wachimbaji; na fursa ya ukodishaji wa mitambo na vifaa chini ya usimamizi wa STAMICO.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles