MAHAKAMA YAOMBWA KUMPIMA DNA ANAYEDAIWA KUZAA NA MCHUNGAJI MWINGIRA

0
901

NA KULWA MZEE

DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeombwa kuamuru Mchungaji Joseph Mwingira wa Kanisa la Efatha, mke wa mtu anayedaiwa kuzaa naye, mtoto na mume halali wakapime DNA ili kujua mtoto ni wa nani.

Maombi hayo yametokana na kesi dhidi ya Mwingira, anadaiwa kuzini na kuzaa na  Dk. Phillis Nyimbi ambaye ni mke wa Dk. William Morris ambaye ni raia wa Marekani amewasilisha maombi mahakamani kwa sababu anadai wawili hao walizini wakazaa mtoto huyo mwenye umri wa miaka tisa sasa.

Morris kupitia wakili wake Respicius Ishengoma aliwasilisha maombi hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, katika maombi hayo namba 113/2017, ambapo baada ya kuwasilisha maombi hayo mahakama imeyapokea na kutoa siku 14 kwa Mwingira kuyajibu kisha usikilizwaji wa maombi uanze na kutolewa uamuzi Agosti 2, mwaka huu.

Katika kesi ya msingi namba 306/2013 Morris amewashtaki Mwingira na mkewe Dk. Phillis, anadai alipwe fidia ya Sh bilioni 7.5 kwa Mwingira kuzini na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mkewe.

Mdai anadai Dk. Nyimbi na Mwingira waliingia katika mahusiano katika muda usiojulikana bila kujali kwamba Nyimbi alikuwa mke wa mdai katika kesi hiyo.

Inadaiwa katika uchunguzi Dk. Nyimbi alidai alibakwa na Mwingira ambapo kubakwa kulisababisha kupata ujauzito na matatizo mbalimbali ya kiafya.

Mdai alifunga ndoa ya kanisani na mkewe Nyimbi Desemba 28 mwaka 2011. Mchungaji Mwingira na Nyimbi waliingia katika mahusiano ya mapenzi na kubahatika kuzaa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here