AKOTHEE ACHANGANYA MASHABIKI

0
581

NAIROBI, KENYA


MSANII wa muziki nchini Kenya, Esther Akoth, maarufu kwa jina la Akothee, amewachanganya mashabiki wake baada ya kusambaa kwa video inayomuonesha akiwa analia barabarani.

Video hiyo inamuonesha msanii huyo akilalamika na kuomba msaada wa kukimbizwa hospitalini kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya miguu.

Baadhi ya mashabiki walijitokeza kwa wingi na kumchukua kisha kumkimbiza hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya, baadhi ya mashabiki wamedai video hiyo ambayo inasambaa si msanii huyo, ila ni dada ambaye amefanana naye.

Hata hivyo, msanii mwenye hajazungumza chochote juu ya taarifa hizo kuwa ni yeye au la na ndipo baadhi ya mshabiki wanapoamini kuwa ni yeye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here