25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 6, 2022

Contact us: [email protected]

Kili Queens yatinga fainali Chalenji

kilimanjaro-queensNa MWANDISHI WETU

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’, jana ilifanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Chalenji) kwa wanawake baada ya kuwachapa wenyeji Uganda mabao 4-1.

Kilimanjaro Queens sasa itacheza mchezo wa fainali dhidi ya Kenya Jumanne, baada ya kuwafunga Ethiopia 3-2 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa Uwanja wa Chuo cha Ufundi Njeru kilichopo mjini Jinja, Uganda.

Katika mchezo wa jana, Kilimanjaro Queens ilianza kwa kishindo na kufunga mabao matatu kipindi cha kwanza, yaliyofungwa na Donosia Daniel dakika ya sita, Mwanahamisi Omari dakika ya 17 na Stumai Abdallah dakika ya 31.

Hata hivyo, dakika chache baadaye, Asha Rashid aliipatia Kilimanjaro Queens bao la nne kabla ya Uganda kupata bao la kufutia machozi.

Kilimanjaro Queens iliyokuwa imepangwa Kundi B kwenye michuano hiyo, ilianza kwa kuichapa Rwanda mabao 3-2 kabla ya kutoka sare ya kutofungana na Ethiopia.

Wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye michuano hiyo ni timu ya taifa ya Zanzibar iliyokuwa imepangwa Kundi A, iliondoshwa kwa aibu baada ya kufungwa jumla ya mabao 30-1 katika michezo mitatu waliyocheza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,606FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles