28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mayanja: Haikuwa kazi rahisi kuifunga Azam

mayanja-j-12Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA msaidizi wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, amekiri kuwa mchezo wao wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ulikuwa mgumu licha ya kuibuka washindi.

Matokeo hayo yaliiwezesha Simba kushika usukani wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 13 kutokana na michezo mitano waliyocheza, wakifuatiwa na Yanga waliojikusanyia pointi 10, huku wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja.

Katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita, mechi kati ya Simba dhidi ya Azam FC, mzunguko wa kwanza ulimalizika kwa sare ya 2-2 na waliporudiana, matokeo yalikua sare ya kutofungana.

Kwa mara ya mwisho kwenye mchezo wa ligi, Simba iliifunga Azam FC mabao 2-1 msimu wa 2014/15, ambapo kwa misimu miwili mfululizo wamekuwa wababe kwa wapinzani wao hao.

Akizungumza baada ya mchezo huo juzi, Mayanja alisema timu zote zilishambuliana kwa zamu kwa kila mmoja kusaka ushindi, lakini bahati iliangukia upande wao baada ya kuitumia vyema nafasi waliyopata.

“Tunashukuru tumepata ushindi muhimu ambao umetuwezesha kuongoza katika msimamo wa ligi, nawapongeza wachezaji kwani walipambana bila kuchoka ili kuhakikisha malengo ya kuondoka na pointi tatu yanatimia,” alisema.

Mayanja ambaye aliinoa Simba msimu uliopita, alisema matokeo waliyoyapata yanaonyesha dalili nzuri ya kufikia mafanikio ya ubingwa msimu huu, ili kutimiza ndoto za Wanamsimbazi kutokana na kushindwa kunyakua taji hilo tangu msimu wa 2011/12.

Kwa upande wake mshambuliaji, Shiza Kichuya, aliyeifungia Simba bao la pekee na la ushindi, aliwaomba mashabiki kuendelea kuiunga mkono timu hiyo ili ifanye vizuri zaidi na kufikia malengo ya kuchukua ubingwa.

Kichuya aliyetua Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, alisema licha ya kuwazidi ujanja wapinzani wao na kuondoka na ushindi, mchezo ulikuwa wa ushindani wa hali ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles