25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI YAIWEKA NMB DARAJA LA KWANZA AFRIKA

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


NMBBENKI ya NMB imewekwa katika daraja la kwanza na kampuni ya kimataifa ya utafiti ya Moody’s Investors Service kwa uwezo wake wa kuhimili madeni na usalama wa kifedha.

Kampuni hiyo ya Moody’s ni moja ya kampuni zinazofanyia tathmini na kushindanisha utendaji wa taasisi za fedha duniani.

Kwa mujibu wa taarifa ya benki hiyo ya NMB kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, daraja hilo linaifanya benki hiyo kuwa ni benki inayoongoza kwa kuwa na huduma bora na za uhakika katika nchi za Afrika isipokuwa Afrika Kusini.

“Benki hii imepata daraja hili baada ya kufanyiwa tathmini katika maeneo mbalimbali ikiwemo mazingira ya uendeshwaji wake, mazingira ya jumla pamoja na shughuli za kibiashara za benki hii,” ilisema taarifa hiyo ya benki.

Kupatikana kwa daraja hilo, kunaendana na malengo ya NMB ya kuhakikisha benki hiyo inakuwa ni taasisi ya fedha inayoongoza kwa kutoa huduma bora nchini.

Aidha, daraja hilo, linaonesha namna pia benki hiyo ilivyo imara na yenye akiba ya kutosha, lakini pia inayozingatia suala la utawala bora.

Bodi ya Wakurugenzi na menejimenti ya benki hiyo, imefurahishwa na kitendo cha benki hiyo kupatiwa daraja hilo, kwani kutaisaidia NMB kuwa katika nafasi ya kujadili masharti mazuri zaidi na watoa mikopo.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Kwa kweli NMB ni benki yangu nnayoipenda,Nawapongeza sana Bodi ya wakurugenzi na wafanyakazi wote,kwa kufanya kazi kwa bidii nakuifanya kuwa benk bora ndan na nje ya nchi.ushauri,sasa ni muda muafaka wa kukaa na kujadili namna ya kushusha kiwango cha riba cha mikopo ili kuifanya taasisi hii kuwa ya kijasiriamal zaidi na zaidi,Evarist frank mshanga,mwl kutoka longido-Arusha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles