22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

MKUU WA MAZINGIRA WA UN AKAGUA MIRADI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


 

MKUU WA MAZINGIRA WA UNMKUU wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP),) Erik Solheim amefanya ziara ya siku mbili nchini ili kuona ushirikiano wa wadau katika utunzaji wa mazingira kwa kutembelea maeneo tofauti Dar es Salaam na Arusha.

Ziara hiyo iliyofanyika juzi, Solheim alitembelea dampo la Pugu Kinyamwezi na kujionea namna uhifadhi na utupaji taka unavyofanyika pamoja na Ubungo alipokutana na kina mama wauza mkaa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juzi, Solheim alisema utunzaji wa taka bado si bora na kwamba anatarajia kuona zikitumika kwa kubadilishwa kuwa nishati ili kutunza mazingira.

“Tunaweza kutengeneza ajira kupitia taka, kubadili taka kuwa nishati hiyo ni njia bora ya utunzaji wa mazingira na kwa pamoja tunaweza, ” alisema Solheim.

Solheim alisema huko Pugu alijionea kiasi kikubwa cha taka ambacho kinatupwa kwa siku takribani Tan 2,000 ambacho hata hivyo alielezwa ni sawa na asilimia 48 tu ya taka hapa jijini.

Alisema aliangalia uwezekano wa kufanya kazi na wadau hapa nchini ili kuzifanya taka kuwa malighafi mbadala pamoja na kuzitenganisha kupata kilicho bora.

Akiwa ubungo alishirikishwa namna kina mama hao wanaouza mkaa wanavyopata kipato kupitia chao ambako alidhamiria kuona namna bora ya kuwawezesha ili kuondokana na ukataji miti hivyo.

Pia katika ziara hiyo ambayo aliambatana na maofisa wengine akiwemo Ofisa Mwakilishi wa Shirika hilo  Clara Makenya, walikutana pia na wadau kutoka taasisi zisizo za serikali zinazojishughulisha na mazingira ili kuona namna bora ya kushirikiana kutunza mazingira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles