RAIS BARROW KUREJEA GAMBIA

0
523

BANJUL, GAMBIA


adama barrowRAIS Adama Barrow anapanga kurejea nchini Gambia baada ya wanajeshi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuimarisha ulinzi nchini hapa.

Barrow alitarajiwa kuwasili nchini hapa wakati wowote kuanzia jana, akitokea nchi jirani ya Senegal, ambako alitafuta hifadhi kwa sababu za kiusalama.

Barrow pia amemteua Fatoumata Tambajang kuwa Makamu wa Rais.

Huo ndio uteuzi wake wa kwanza tangu alipochukua madaraka Januari 19 baada ya mtangulizi wake Yahaya Jammeh kuachia ngazi chini ya shinikizo la kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here