JAY Z: KUDUMISHA NDOA KUNA MAMBO MENGI

0
754

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa muziki wa hip hop ambaye anatamba na albamu yake mpya ya 4:44, Jay Z, ameweka wazi kuwa ili ndoa iweze kudumu lazima kuwe na uongo na ukweli.

Msanii huyo ambaye amefunga ndoa miaka tisa iliyopita na mke wake Beyonce, amedai kuwa hakutumia ukweli kwa asilimia 100 ili kumshawishi mke wake huyo kufunga ndoa, kuna wakati alilazimika kuwa muongo ili kufanikisha mipango yake.

“Huu ni ukweli juu ya ndoa yangu, ni kwamba sikuwa mkweli kwa asilimia 100 ili kumshawishi Beyonce kufunga ndoa na mimi, kuna wakati nilikuwa muongo ili aweze kunielewa na hatimaye leo hii tupo hapa.

“Misukosuko ndani ya ndoa ni kitu cha kawaida, kikubwa ni uvumilivu na kutosikiliza mambo ya pembeni, ukiyapa nafasi mambo ya pembeni ni rahisi ndoa kuvunjika, kwa sasa tunafurahia maisha ya pamoja kwa kipindi cha zaidi ya miaka tisa,” alisema Jay Z.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here