SHAMSA FORD ANAHITAJI WATOTO WANNE ZAIDI

0
1219

Na KYALAA SEHEYE


MKE wa mfanyabiashara wa nguo, Rashid Said (Chid Mapenzi), Shamsa Ford, ameweka wazi kwamba baada ya kuishi katika ndoa kwa muda mrefu sasa anataka watoto wengine wanne.

Msanii huyo ambaye alifunga ndoa Septemba mwaka jana, aliliambia MTANZANIA kwamba ameshafanya mambo mbalimbali ya starehe na mume wake huyo na sasa umefika wakati wa kuongeza watoto wengine wanne ili idadi yao wawe watano.

“Kama kupendana tunapendana, hivyo tunahitaji kupata watoto wanne zaidi katika ndoa yetu ili tuongeze furaha ya ndoa na watoto hao nitawazaa haraka haraka ili niendelee na majukumu mengine ya kimaisha,” alisema Shamsa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here