26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

HUDDAH MONROE ATANGAZA KUMRUDIA MUNGU

NAIROBI, KENYA


STAA wa mitindo ambaye hakauki kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya, Huddah Monroe, ameweka wazi sababu ya kufuta picha zake kwenye akaunti ya Instagram na kukaa mbali na mitandao ni kuwa anataka kumrudia Mungu.

Mrembo huyo aliwashangaza mashabiki wake milioni 1.2 kwenye akaunti hiyo, lakini ameamua kufunguka na kusema, wala akaunti yake haijadukuliwa kama ilivyo awali, lakini kwa sasa ameamua kufanya hivyo kwa ajili ya kumpa nafasi Mungu.

“Akaunti yangu bado ni salama wala haijadukuliwa, lakini nimeamua kufuta kusudi kwa sababu nataka kumtafuta Mungu kabla ya kujitafuta mimi mwenyewe.

“Mbali na kufuta baadhi ya picha zangu, lakini nimeamua kukaa mbali kidogo na mitandao ya kijamii, kila kitu kina wakati wake,” alisema Huddah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles