30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

KANGI: TUTAWAFUNGA WABUNGE WATAKAOKWAMISHA MRADI WA STIGGLER’S GORGE

Maregesi Paul, Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Kangi Lugora amesisitiza kwamba serikali iko tayari kuwafunga jela wabunge watakaokwamisha mradi wa Stiggler’s Gorge.

Akijibu hoja za wabunge zilizoelekezwa katika wizara yake katika bajeti ya Wizara ya Nishati bungeni jijini Dodoma leo, Kangi amesema pamoja na malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wabunge kwamba mradi huo haujafanyiwa tathmini ya mazingira, serikali imeshafanya tathmini hiyo kwa kuwashirikisha wataalamu mbalimbali.

“Wabunge naomba tushirikiane na serikali katika kutekeleza mradi huo kwa kuwa una manufaa kwa taifa,” amesema.

Hata hivyo, majibu hayo ya Kangi yalionekana kuwakera baadhi ya wabunge wa upinzani na kulazimika kupiga kelele za kuzomea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles