31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri yaweka mikakati ya kukusanya mapato ya ndani

Na Malima Lubasha, Serengeti

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, limepitisha mapendekezo ya bajeti ya zaidi ya Sh bilioni 48.9 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kuweka mikakati ya kukusanya mapato ya ndani.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ayubu Makuruma amesema hayo katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kupitisha bajeti ambapo kati fedha hizo Sh bilioni 44 ni ruzuku kutoa Serikali Kuu ikiwa ni ongezeko la Sh bilioni 7.9 ukilinganisha na bajeti Sh bilioni 41 ya mwaka fedha 2023/20 24.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

Makuruma alibainisha kuwa mapato ya ndani wanatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 4.7 kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 na kubainisha vyanzo vipya vya mapato wanakwenda kuvuka lengo hilo kutokana na mikakati kabambe waliyojiwekea kwa mwaka huu wa fedha kutokana na kupoteza mapato mengi kwa sababu baadhi ya watumishi wasio waadilifu kutumia mapato wanayokusanya kwa manufaa yao binafsi hivyo kukwamisha maendeleo.

“Hatuwezi kuacha mapato yetu yanapotea bila utaratibu na hatutamvumilia mtumishi mzembe lazima Mkurugenzi wa Halmashauri aende afanye mapinduzi makubwa katika idara yake ya manunuzi kuhakiki sha suala la ukusanyaji mapato linapewa kipaumbele zaidi kuliko kuacha yanapotea wakati wananchi wetu hawana maji, huduma za afaya pia wanakosa mikopo ya asilimia kumi kwa sababu ya uzembe wa watu wachache,” amesema Makuruma.

Tunaagiza Mkurugenzi uandae timu ya kukusanya mapato ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwenye ushuru wa huduma ambao taasisi husika wamekuwa wakichelea kulipa.
Amesema wengine ni mashirika ya ndege yanayo fanya kazi ndani ya hifadhi hiyo, wamiliki wa magari ya kubeba wageni ndani ya hifadhi nao lazima walipe mapato katika halmashauri yetu.

Mwenyekiti Makuruma alifafanua kuwa Madiwani wako tayari kwenda mstari wa mbele kwenda kusaidi a kukusanya mapato kama timu yako itashindwa kufanya hivyo,kwani wametunyonya kwa muda mrefu bila kupata mapato yetu alihoji kwa nini wanakwenda kulipia mkoani Arusha wakati huduma zinafanyi ka wilaya ya Serengeti.

Naye Mbunge wa Jimbo la Serengeti Dk. Amsabi Jeremia Mrimi amesema muda umefika halmashauri kuchukua hatua kali dhidi ya wote wanao kwepa kulipa mapato ya ushuru wa huduma ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa halmashauri yetu kwa sababu jambo hili limekuwa likizungumziwa kila mwaka na kupuuzwa bila kufanyiwa kazi.

“Hatuko tayari kumvumilia yeyote atakaye kaidi kulipa mapato ndani ya halmashauri yetu lazima tuchukue hatua kwani mapato yapo mengi ndani ya hifadhi wakati sisi tunakosa mapato hili halikubaliki kabisa nawataka wataalam na madiwani kushikamana ili waweze kupata mapato makubwa ya ndani ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo,” amesema Dk. Amsabi Mrimi.

Baraza hilo lilijadili hali ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri, bajeti na kupendekeza njia bora za kudhibiti upotevu wa mapato huku mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Afraha Hassan akiahidi kutekeleza maazimio yote na kufanya mabadiliko makubwa ya ukusanyaji mapato.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles