24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

HAKIMU KESI YA LEMA AGOMA KUJITOA

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya  Arumeru, Desderi Kamugisha amegoma kujitoa katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Lema kupitia mawakili wake, amemtaka hakimu huyo kujiondoa katika kesi yake kutokana na kutokuwa na imani naye kwa sababu mbili ikiwamo kumnyima dhamana wakati ilikuwa wazi hatua iliyosababisha Lema kukaa mahabuzu zaidi ya miezi mitatu.

Akijibu maombi hayo,  Hakimu Kamugisha amesema haoni sababu ya kujitoa na kesi hiyo itaendelea mbele yake kwani kilichotokea ni makosa ya kawaida ya kisheria.

“Jaji au hakimu hatakiwi kujiondoa katika mashauri kwa sababu za kufikirika ingawa anaweza kufanya makosa ya kisheria na mtu anaweza kukata rufaa lakini hilo haliwezi kumfanya akajitoa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles