GIDEON MOI: KURA ZA BONDE LA UFA NI ZA UHURU

0
641

NAIROBI, KENYA


SENETA wa Kaunti ya Baringo Gideon Moi amemhakikishia Rais Uhuru Kenyatta kuwa atavuna kura nyingi kutoka Bonde la Ufa.

Seneta huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama kilichoasisi uhuru wa Kenya, Kenya African National Union (KANU) amesema amejitoa mhanga kumpigia debe Rais Kenyatta katika eneo la Bonde la Ufa ili achaguliwe katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8.

“Mimi ni Mkalenjin, jana (Jumamosi) nilikuwa huko (maeneo ya Bonde la Ufa) na mambo si mabaya kwake Rais Kenyatta," alisema Moi wakati akihutubia Limuru, Kaunti ya Kiambu.

Mei mwaka huu chama cha KANU kilitangaza rasmi kumuunga mkono Rais Kenyatta Agosti 8 na kuahidi kumfanyia kampeni.

“Sisi KANU tuliamua 'tuko ndani' na Rais Uhuru Kenyatta. Tuliamua kwa sababu ya kitu kimoja; tunataka amalize kutekeleza miradi yake ya maendeleo aliyotuahidi tunaona inabadilisha maisha ya Wakenya. Tumpe hiyo nafasi tena Agosti 8 abadilishe maisha yetu," alisema Moi.

Mtoto huyu wa Rais Mstaafu Daniel Arap Moi, pia amewataka wapiga kura kumrudisha tena katika useneta wa Kaunti ya Baringo.

Licha ya kumpigia kura Kenyatta, lakini Seneta Gideon haivi chungu kimoja na Naibu Rais William Ruto, ambaye wamekuwa wakishindana juu ya nani kati yao mwenye ushawishi mkubwa kwa jamii ya Wakalenjin kati Bonde la Ufa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here