29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

FAAY BABY: NAMHITAJI BARNABA

MREMBO chipukizi kwenye muziki wa Bongo Fleva anayefanyia kazi zake visiwani Zanzibar, Faidha Iddi ‘Faay Baby’, ameweka wazi hamu yake ya kukutana na kufanya kazi na wasanii wawili akiwemo Elias Barnaba kutoka Tanzania Bara.

Mrembo huyo aliyefanya shoo nzuri kwenye Tamasha la Zanzibar Swahili, alisema amekuwa na hamu kubwa na ya muda mrefu ya kufanya kazi na Barnaba kwa madai kwamba anapenda muziki wake na namna anavyopiga gitaa kwa uhodari wa hali ya juu.

“Kuna mtu ananifanyia mpango nikutane na Barnaba kwenye studio yake ya High Table na imani yangu ni kwamba nitakutana naye na tutafanya kazi nzuri, lakini pia natamani kufanya kazi na msanii mwingine wa hapa Zanzibar anaitwa Smile ambaye nimeshakutana naye na kuzungumzia kazi hiyo,” alieleza Faay Baby.

Faay Baby kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Basi Nipende’ lakini ameshatoa nyimbo nyingine mbili ukiwemo ‘Umejivuruga’ na ‘Simanzi’ ambao ameshirikiana na msanii wa Zanzibar, Sultan King.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles