27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WENGER: TOP FOUR INATUHUSU

LONDON, ENGLAND


BAADA ya klabu ya Arsenal kushinda mabao 2-1 juzi dhidi ya Middlesbrough katika michuano ya Ligi Kuu nchini England, kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, amedai ‘Top Four’ bado inawahusu.

Kocha huyo amesema bado wana nafasi hiyo ya kuingia katika nafasi nne za juu endapo watapambana na kushinda michezo yote iliyobaki.

Hadi sasa wamebakiwa na michezo saba kuweza kumaliza ligi, hivyo Wenger amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanaendelea kushinda katika kila mchezo ili waweze kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Katika msimamo wa ligi, Arsenal inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza michezo 31, wakati huo vinara wa ligi hiyo, Chelsea, wakiwa na pointi 75 baada ya kucheza michezo 32.

“Lengo letu kwa sasa ni kuhakikisha tunapambana ili kuweza kuingia nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi, ushindani ni mkubwa sana na kila timu ipo kwenye mipango hiyo ya kuwania nafasi za juu na kama si kuwania ubingwa.

“Kazi tuliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo kati ya saba iliyobaki ili kuingia katika nafasi ambayo tunaitolea macho na tuweze kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Nadhani timu kwa sasa inarudi katika kiwango chake, tumeweza kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Middlesbrough na kama hali itaendelea hivyo, basi bado tuna nafasi ya kuingia katika top four kutokana na mahesabu rahisi ambayo unaweza kuyafanya, tunajua kuwa ni ngumu lakini tunaamini inawezekana hivyo ni lazima tupambane,” alisema Wenger.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na washambuliaji wake ambao hadi sasa hawataki kuongeza mikataba mipya, Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

Mbali na ushindi huo wa juzi lakini bado mashabiki wa Arsenal walionekana uwanjani, huku wakiwa na mabango ya kumtaka kocha huyo aondoke mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Kuna tetezi zinasema kuwa uongozi wa klabu hiyo tayari umekaa na kocha huyo na kutaka kumuongezea mkataba wa miaka miwili japokuwa mashabiki hawamtaki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles