Erick Kisindja asaidia watoto yatima

0
571

NAIROBI, KENYA

MTUMISHI wa Mungu ambaye pia ni mwimbaji wa Injili nchini Kenya, Bishop Erick Kisindja kupitia taasisi yake ya Jesus Temple Ministry For All Nations, ametoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima jijini Nairobi.

Akizungumza na MTANZANIA, Bishop Kisindja alisema lengo la taasisi hiyo ni kusaidia watu wenye uhitaji kwenye jamii kama yatima, wajane na watoto wa mtaani.

“Jesus Temple Ministry For All Nations tumeanza kugusa maisha ya watu kwa kusaidia yatima, tutaendelea kufanya kazi hii ya Mungu ili tuwafikie watu wote wenye uhitaji ndani na nje ya Kenya,” alisema Kisindja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here