28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mashinji aagiza wananchi wasiohudhuria mikutano kuchukuliwa hatua Serengeti

*Ni baada ya mkutano kuhudhuriwa na watu chini ya 20

*Ataka sheriz ndogo za vijiji zitumike kuwabana

Na Malima Lubasha, Serengeti

VIONGOZI wote wa Serikali za vijiji katika Wilaya Serengeti mkoani Mara, wametakiwa kutumia sheria ndogo za vijiji kuwachukulia hatua wananchi wanaokaidi kuhudhuria mikutano bila sababu badala yake wanalalamika kutosomewa taarifa ya mapato na matumizi.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dk. Vicent Mashinji ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Robanda alipofika kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ambapo mahudhurio yao hayakumlidhisha kiongozi huyo na kuagiza uongozi wa kijiji kupita kila nyumba kuwakamatia wasiohudhuria na fedha zote zitakazopatikana ziende kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akitoa msimamo wa wilaya alisema siku mbili kabla kikao hicho cha kijiji alihudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti wakiwasilisha taarifa zao madiwani walidai kuwa kata 30 zilizopo ni kata 7 ndizo wananchi hawahudhurii mikutano inayoitishwa na serikali za vijiji na kutaja kata ya Ikoma yenye vijiji 2 ikiwa moja wapo wananchi hawahudhurii mikutano.

Dk. Mashinji alisema kufuatia malalamiko hayo kutolewa na madiwani kabla alikwenda kijiji cha Parknyi goti kusikiliza kero za wananchi waliodai hawajasomewa taarifa ya mapato na matumizi ambapo alitoa siku 7 kuitisha kikao cha kusomewa taarifa hiyo lakini wananchi waliohudhuria walikuwa 34 wakaitisha tena waliofika walikuwa 50.

Alisema kuwa kama hiyo haitoshi alikwenda katika kijiji hicho akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda wananchi walilalamika hawasomewi taarifa ya mapato na matumizi akaagiza wasomewe tena ambapo siku hiyo walivunja rekodi kwani waliofika walikuwa ni chini ya watu 20.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kijiji hicho chenye zaidi ya kaya 500 alitarajia wangehudhuria zaidi ya watu elfu moja lakini wanaohudhuria ni watu 20 hivyo aliagiza serikali ya kijiji kuitisha kujadili hali hiyo na kuhoji kwa nini wananchi hao waliokaidi wasiitwe waeleze kwa nini hawahudhurii vikao na wasichu kuliwe hatua ilikukomesha hali hiyo.

“Kijiji cha Robanda kina kaya zaidi 600 watu hawakutani kujadili maendeleo yao badala yake ni kulalami kwamba hawasomewi mapato na matumizi, mimi hii ni mara pili kuitisha kikao nilitarajia leo watu 1,200 wange kuwa hapa hivyo naagiza wasiohudhuria kwa hiari yao ndani ya siku saba wapeleke shilingi 5,000/- kwa mtendaji wa kijiji, naagiza tena wiki ijayo siku ya Jumatano taarifa hiyo isomwe mbele ya wananchi,” amesema Dk. Mashinji.

Katika kusikiliza kero za wananchi mkazi mmoja wa kijiji hicho, Joyce Mabenga aliomba zahanati yao ipandishwe hadhi kuwa kituo cha afya kwani eneo hilo lina hoteli nyingi za kitalii ambapo watalii kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakitembelea kijiji hicho mara kwa mara wakati wa msimu wa utalii na pia wananchi wenyewe watapata huduma bora zaidi za matibabu ombi hilo lilipokelewa na serikali ya wilaya na kuahidi kulifanyia kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles