31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Washindi 56 wa Mtoko wa Kibingwa kushuhudia Derby ya Kariakoo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI namba moja ya michezo ya kubashiri nchini Betika imezindua rasmi Kampeni yake kubwa ya “Mtoko wa Kibingwa” kwa Msimu wa 7 kwa wateja wake na kuendelea kutimiza ndoto za mashabiki wa soka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Februari 19,2024 Afisa Habari wa Betika, Rugambwa Juvenalius amesema Kampeni hiyo imezinduliwa leo ambapo droo zitaanza Februari 27,2024 hadi kufikia tamati Aprili 10,2024 na Mabingwa 56 kushuhudia derby ya watani wa Jadi kati ya Yanga na Simba katika Jukwaa la VIP A.

Aidha, Juvenalius ameeleza sababu ya kuwepo kwa Kampeni hiyo kuwa inalenga kuwaleta pamoja mashabiki wa soka na kuwapa fursa ya kufurahia burudani ya kipekee ya kushuhudia mechi ya watani wa jadi bila longolongo.

“Kampuni yetu ya Betika katika mtoko huu wa Kibingwa itahakikisha inatoq zawadi za wiki, za mwezi pamoja na Usafiri wa Tiketi za Ndege kwa washindi watakaopatikana mikoani na gharama za kila kitu zitalipwa na sisi wenyewe betika,” amesema.

Pia amesema kampeni hiyo inamuhitaji mshiriki abashiri kwa mikeka mitatu ambapo dau lake ni Sh 2,000 tu.

“Mshiriki atatakiwa kuweka ubashiri kwa dau la 2,000 mechi zaidi ya 3 anaingia kwenye droo ya ushindi,” amesema na kuongeza kuwa:

“Hata hivyo, watakaobashiri mara nyingi zaidi kwa wiki na kutofanikiwa kushinda mikeka hiyo watapata zawadi ya simu Android wakati watakaobashiri zaidi kwa mwezi watajishindia simu aina ya Iphone 15.

“Kumbuka mkeka utiki au usitiki unaingia kwenye droo ya kushinda mtoko wa kibingwa hivyo waendelee kuweka ubashiri wao kupitia www.betika.co.tz au piga 14916#,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles