23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Dk Gwajima azindua mwongozo kuzuia ukatili wa kijinsia

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk Doroth Gwajima amezindua mwongozo wa mgawanyo wa majukumu wenye kipengele cha kuzuia ukatili wa kijinsia huku akisisitiza jamii ina wajibu wa kuondoa aina zote za ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.

Akizungumza leo Septemba 29,2021,Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi huo ambao ulihudhuriwa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini,Waziri Gwajima amesema mwongozo huo utasaidia kupambana na changamoto ya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Waziri huyo ametoa wito kwa watumishi wa kada ya afya kuusoma ili wauelewe mwongozo huo ambapo amedai suala la ukatili wa kijinsia bado ni tatizo katika jamii hivyo zinahitajika juhudi za pamoja kutokemeza jambo hilo.

Waziri Gwajima amesema mila na desturi potofu bado zipo katika jamii hivyo kila mmoja anatakiwa kupambana kuhakikisha tatizo hilo linaondoka.

Amesema ili kukabiliana na jambo hilo zinahitajika mbinu za ushirikiano katika makundi yote,kuondoa aina zote za ukatili wa kijinsia,kuzuia aina mpya na ya  zamani kujitokeza pamoja na elimu endelevu kwa jamii.

Waziri huyo amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa ushahidi pindi watuhumiwa wanapopelekwa katika vyombo vya sheria.

Naye,Mwenyekiti wa Tanzania Interfaith Patnership (TIP) Sheikhe Khalid Mfaume amesema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinakadiria takribani wasichana milioni 150 na wavulana milioni 73 chini ya miaka 18 wameishafanyiwa vitendo mbalimbali vya ukatili na udhalilishaji.

Amesema jambo hilo ni changamoto ambayo sio ya kufumbiwa macho kwani maendeleo endelevu hupatikana kwa kuweka mazingira mazuri kwa watoto.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano wamejikita katika mambo yanayohusu ushawishi wa kusimamia mambo ya watoto malezi na usafi ambapo mwaka huu wanatarajia kutanua zaidi huduma kufikia ulinzi  wa mtoto na kusimamia masuala ya lishe kwa mtoto.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)Jabir Mruma amesema wameendelea kutoa elimu kwa waumini wa dini ya kiislamu kuhusiana na umuhimu wa chanjo ya ugonjwa wa Uvico 19.

“Tumeendelea kutoa elimu juu ya chanjo ya ugonjwa wa Uvico 19 na sisi tumechanja na tupo vizuri ,sisi viongozi wa dini tutaendelea kushirikiana na Serikali yetu katika mambo mbalimbali,”amesema  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles