31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Wizara. Mashirika yajipanga kutoa elimu chanjo ya Uviko -19

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dk.Doroth Gwajima ameyataka Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali kushirikiana na Serikali kufikisha elimu  ya chanjo ya Uviko 19 kwa wananchi  huku akisisitiza chanjo hiyo ni ya hiari kama alivyosisitiza Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza leo Septemba 29,2021 Jijini Dodoma wakati akifungua semina elekezi kwa viongozi wa Mashirika Yasiyoyakiserikali (NG’Os),Waziri Gwajima amesema wanatambua kazi kubwa inayofanywa na mashirika hayo ambapo amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu juu ya chanjo ya Uviko 19.

Waziri Gwajima amesema suala la chanjo ni  hiari na Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza katika mikutano yake hivyo Mashirika hayo yanawajibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na jambo hilo.

“Napenda kusisitiza pia na kuwakumbusha  kwamba chanjo hii ni  hiari na Mheshimiwa Rais amekuwa akikumbusha   kila mara  anapokwenda  kwenye  mikutano yake na kuwakumbusha watanzania wajitokeze wakachanje kwa hiari.

“Nia yake Rais ni kuona Taifa lipo salama na Uviko 19 kwa kutekeleza afua za kinga ikiwemo afua ya chanjo kwa hiari dawa ya hiari ni elimu amesema Rais wetu elimu ya kutosha hili amelisisitiza.

Hivyo nitumie nafasi hii kuwakummbusha nyinyi kama wadau wenye majukumu mbalimbali na uelewa wenu  mkubwa na uzoefu wenu mkashirikiane na wataalamu wetu wa afya na sekta zote mkasimamie na kuwezesha suala la elimu.

“Elimu  itolewe kwa wananchi na suala la  dhana ya uhiari likafanyike vizuri kwa kuwekeza kwenye msingi wa elimu kama alivyosema mheshimiwa Rais.

“Ikatokea mahala watu wengine wakataka kupotosha nia njema ambayo Rais amesema bahati nzuri wale watu wakaomba msamaha tulishasema ‘speech’ za viongozi ni suala nyeti kabla hujaamua kutoka nayo hakikisha umeilewa,”amesema.

Aidha,Waziri Gwajima amewashukuru wananchi kwa jinsi ambavyo wameipokea kampeni hiyo ambapo amedai Serikali itaendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa huo.

“Wizara itaendelea kushirikiana nanyi katika kutekeleza dhamira kubwa ya Rais ya elimu kukubaliana na Uviko 19.Mashirika yasiyokuwa yakiserikali mshirikiane na kule chini ili kila sikio likasikie ili kutekeleza afua hii,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles