STAA wa ndondi duniani, Manny Pacquiao, ametangaza kustaafu mchezo huo akiwa na umri wa miaka 42, lengo kubwa la kufanya hivyo likiwa ni kuelekeza akili kwenye kinyang’anyiro cha urais nchini Ufilipino.
“Nikiwa naachana na masumbwi, ningependa kuushukuru ulimwengu mzima, hasa watu wa Ufilipino kwa kumsapoti Manny Pacquiao. Kwaheri ndondi,” ameandika bondia huyo kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Kwa miaka 26 aliyopanda ulingoni, amedundwa mapambano nane tu kati ya 72 aliyopigana, akishinda 62 na sare mbili.
Katika pambano lake la mwisho, bondia huyo ambaye ni seneta huko Ufilipino, alitandikwa na Yordenis Ugas na hiyo ilikuwa Agosti 21, mwaka huu.