24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

DENI LA BIL 2/- LAKOSESHA WANANCHI MAJI

NA FLORENCE SANAWA, TANDAHIMBA


MKUU wa Wilaya ya Tandahimba, Sebastian Waryuba, ameitaka halmashauri hiyo kuhakikisha wanafanya mikakati ya kunusuru tatizo la maji, baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Makonde Platue kukatiwa huduma ya umeme na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

 Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo jana, Waryuba alisema mamlaka hiyo inadaiwa zaidi ya Sh bilioni 2.

Alisema kitendo hicho kimesababisha  halmashauri zaidi ya tatu kukosa huduma hiyo, hali ambayo imeongeza hofu kutokana na kutokuwa na uhakika wa mamlaka hiyo kurudishiwa huduma.

“Kitendo cha halmashauri tatu kutegemea mamlaka moja kutoa huduma kinaweza kutuweka katika wakati mgumu, madiwani wanapaswa kujipanga ili kupata suluhu itakayowapa uhakika wa huduma ya maji ya uhakika kwa Wilaya ya Tandahimba.”

Naye Diwani wa Kata ya Chingungwe, Ismail Nankuna (CCM), alisema kitendo cha mamlaka hiyo kukatiwa maji kinaweza kuongeza tatizo kutokana na wananchi wengi kutumia maji ya visima.

“Sisi kinachotusaidia ni hivi visima vya kuvuna maji ambavyo tunavyo majumbani mwetu, tungekuwa na hali mbaya zaidi, yapo maeneo yanahitaji maji mengi zaidi tunapaswa kuyaangalia ili tuyanusuru,” alisema Nankuna

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba, Said Msomoka,  alisema kukosa huduma hiyo kumesababisha hali kuwa mbaya.

Alisema sasa wamejipanga kuangalia vyanzo vya maji vya ndani ya halmashauri ili kutatua tatizo hilo.

“Hali ya maji ni mbaya katika halmashauri yetu, deni la mamlaka ni kubwa, ndiyo maana tumeanza mikakati ya kuhakikisha tunalitatua kupitia vyanzo vyetu vya ndani, mvua ndiyo inatuokoa,” alisema Msomoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles