30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MBEGU BORA

NA RAYMOND MINJA -IRINGA


WAKULIMA wadogo wameshauriwa kujenga utamaduni wa kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti  wa kitaalamu ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na kuifanya kazi hiyo kuwa na tija.

Ushauri huo ulitolewa jana na Ofisa Masoko wa Kampuni ya Pannar  (Pannar Seed Tanzania LTD) ya jijini Arusha, Sabasaba Manase, wakati akizungumza na wakulima wa vijiji vya Lugodalutali, Sadani na Mapogolo, wilayani Mufindi.

Alisema wakulima wanayo nafasi ya kuongeza tija katika sekta hiyo kwa kuhakikisha wanalima shamba wanaloweza kulihudumia na kwa kutumia mbegu bora, mbole na kulisafisha kwa wakati.

“Sisi tunachotaka muondokane na kilimo cha mazoea, badala yake muendesha kilimo chenye tija, watumieni pia maofisa ugani walipo kwenye maeneo yenu, kwa kufanya hivyo mtafanikiwa tu,” alisema.

Alisema zipo aina tofauti za mbegu ambapo ni zile zinazokomaa kwa muda mrefu na ni mahususi kwa wanaolima maeneo yenye mvua nyingi.

Kwa upnde wake, mkulima wa Kijiji cha Mapogolo, Baltazar Antony, alishukuru kampuni hiyo kufika vijijini kuwapa elimu wakulima na kuomba kampuni hiyo kushirikiana na serikali kuanza kazi ya usambazaji wa mbegu kwa wakati.

Naye Aidan Lunyungu, mkulima kutoka Kijiji cha Lugodalutali, aliwashauri wakulima wenzake kubadilika na kuanza kutumi mbegu za kisasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles